Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Friday, May 04, 2018

Saturday, December 23, 2017

Saturday, June 24, 2017

Rayvan Ajinyakulia Tuzo Best International Views Choices  (BET)

Rayvan Ajinyakulia Tuzo Best International Views Choices (BET)

Image result for picha za rayvanny

Msanii anaewakilisha label ya WCB  Wasafi Rayvany  ameingia katika Historia ya Muziki wa Tanzania mara baada ya Kufanikiwa  kushinda Tuzo ya  Best International Views Choices ya BET,  Tuzo hizi zilikuwa zinafanyika huko nchini Marekani.

 mwimbaji huyu jina lake lilitajwa kuwa ni moja ya majina yanayowania tuzo za BET 2017 Marekani ambapo alitajwa kuwania tuzo kwenye kipengele chaBest International Views Choices. Rayvanny ni msanii pekee kutoka Afrika kuwania tuzo hiyo ambayo ilimpambanisha na wasanii wengine sita kutoka Marekani, Ulaya na Asia.

Kupitia ukarasa  wa  Instagram wa   Diamond Platnumz ambaye ndiye Boss wa WCB Ameandika hivi‘rayvany is the Best viewers Choice Best International Act  2017  WOOOOYOOO nikishindwa na mkono wa Kulia, ntatumia mkono wa Kushoto ...ila lazima ifike  WCB_WASAFI TANZANIA Chukua hiyo’

Hongera sana kwa Rayvany Bila shaka Ushindi wake ni elimu nzuri kwa  wasanii  wachanga kwakuwa  safari ya  Rayvany hadi kufika  alipo  haikua ndogo.

Endelea kufatilia chotamtemi.blogspot.com tutakujuza mengi zaidi

Saturday, May 20, 2017

Wolper afunguka kuachana kwake na Harmonize

Wolper afunguka kuachana kwake na Harmonize


Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amedai aliachana na aliyekuwa mpenzi wake Harmonize miezi 3 iliyopita lakini waliamua kuficha kwaajili ya shughuli zao za kibiashara.

Muigizaji huyo ambaye alicheza vitendo kwenye video ya wimbo ‘Niambie’ wa Harmonize, amedai wakati kazi hiyo inatoka walikuwa tayari  wameachana lakini waliamua kushirikiana katika promo ya wimbo huo ambao unafanya vizuri.

“Nyie mnajua sisi tumeachana juzi? Tumeacha miezi mitatu iliyopita kabla hata ya wimbo wake Niambie haujatoka,” Wolper alikiambia kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV.

Aliongeza ,“Sisi wenyewe tuliamua kukaa kimya kwa sababu kuachana sio kugombana kuna kesho mnaweza kushirikiana katika mambo mengine ya kibiashara,”

Hata hivyo muigizaji huyo aligoma kueleza sababu ya kuachana na muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Happy Birthday’.

Wednesday, March 15, 2017