Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Friday, August 31, 2018

Bob Wine akamatwa tena

Bob Wine akamatwa tena




Mbunge wa Upinzani nchini Uganda ambaye pia ni mwanamuziki Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine ambaye anadaiwa kupigwa na kuteswa baada ya kukamatwa mapema mwezi huu, inasemekana amezuiwa kuondoka kwa ajili ya kwenda kupata matibabu nje ya nchi.

Akizungumzia kukamatwa kwa mteja wake, Mwanasheria wa Mbunge huyo Robert Amsterdam amesema Bobi Wine alizuiliwa kuingia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Uganda na kuchukuliwa na polisi ambao wanadaiwa kumpeleka katika hospital ya serikali.

''..licha ya kwamba Jaji alitaka apewe pasi yake ya kusafiria kwa sababu anahitaji kuondoka nchini humo kwa sababu ya kwenda kupata matibabu nje, kufuatia mateso makali ambapo yeye na wabunge wengine 33 wa upinzani waliyapata, amechukuliwa kikatili na gari la wagonjwa la polisi, Mawakili hawajui wapi alipopelekwa na tumepatwa na mshtuko..'' Alisema wakili wa Bobi Wine

Kabla ya Kuzuiliwa kwa Bobi Wine, mbunge mwingine tena wa upinzani Francis Zake pia alizuia Uwanja wa ndege kwa ajili ya kwenda kupata matibabu nje ya nchi.

Bobi Wine anakabiliwa na makosa ya uhaini, kufuatia tukio la kushambuliwa kwa mawe gari la Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni. Aliachiliwa kwa dhamana kutoka kizuizini alikokuwa akishikiliwa siku ya Jumatatu, akiwa katika hali mbaya.

Mwanasheria wake Robert Amsterdam anasema kipaumbele cha Bobi Wine ni kupata matibabu na si kuitoroka nchi.

Source BBC

Tuesday, June 12, 2018

Donald Trump na Kim Jong Un wakutana Uso kwa Uso Singapore

Donald Trump na Kim Jong Un wakutana Uso kwa Uso Singapore

Trump na Kim wameshikana mikono kwa tabasamu

Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore.

Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili hao pekee na wakalimani wao. Kwa sasa, viongozi hao wanakula chakula cha mchana.

Mkutano huu ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.

Trump alisikika akisema kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa haikuwa rahisi kufika hapo.

Mkutano uliokua ukisubiriwa kwa hamu na ghamu ulifanyika katika Hotel ya Capela katika kisiwa cha utalii cha Sentosa.

Viongozi hawa wakiingia katika mkutano walionekana wenye tabasabu, na kusalimiana kwa kushikana mikono, na baadae Kim Jong Un alimshika bega Trumpa kisha wakaanza kuzungumza kwa msaada wa wakalimani wao.

Baadaye washauri na maafisa mbalimbali walitarajiwa kuingia kuendelea na mkutano huku suala la nyuklia likitarijiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana bado makubaliano yatakua yapi.

Akizungumza kabla ta mkutano , katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa umoja wa mataifa utatoa msaada wowote wa kuhamasisha makubaliono katika mkutano huo.

''Viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndio vinabaki kuwa lengo kuu, kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakua na changamoto za hapa na pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote," alisema Guterres.

Mcheza kikapu wa zamani wa NBA, Dennis Rodman amefika Singapore asubuhi ya leo kwa ajili mkutano huo, Rodman ambaye ni rafiki wa kiongozi wa Korea Kaskazini amesema kuwa anafurahia kufika na kushuhudia mkutano huo wa kihistoria.

Source BBC

Monday, May 28, 2018

HII NDIO IRAN YA MASHARIKI YA KATI.

HII NDIO IRAN YA MASHARIKI YA KATI.



Iran ni moja kati ya nchi takribani 17 zinazopatikana mashariki ya kati, inayoundwa na sehemu kubwa ya Asia ya magharibi pamoja na Afrika ya Kasikazini, huku Teheran ukiwa ndio  mji mkuu wa  nchi hiyo na lugha rasmi ni lugha ya kiajemi (Farsi).


Irani imekuwa huru tangu kutokea mapinduzi  ya kiislamu  mwaka 1979 yaliyoangusha utawala wa kifalme, jina  Irani lilichukuliwa kuwa jina rasmi la nchi hiyo badala ya  Persia,  kabla ya kuwa jamhuri ya kiislamu ya Irani baada ya mapinduzi  ama Uajemi jina ambalo limejulikana tangu kale.
Mamlaka kuu ya nchi hiyo iko mikononi mwa kiongozi mkuu wa mapinduzi ambaye huchaguliwa na mkutano wa wataalamu wa uongozi kwa muda wa maisha yake, anayesimamia siasa ya nchi kwa jumla, aidha kiongozi huyo ana mamlaka ya kuweza kumwachisha urais rais wa nchi hiyo, ambapo Ayatollah Khamenei ni kiongozi wa pili tangu mapinduzi ya kiislamu.
Serikali inayoongozwa na rais wa Uajemi ambaye ana nafasi ya pili baada ya kiongozi mkuu. Huchaguliwa na wananchi wote  kwa kipindi cha miaka minne na anaweza kuchaguliwa tena, aidha rais anaongoza serikali na kazi yake akiwa chini ya kiongozi mkuu.
Baada ya mapinduzi uislamu wa kishia  ulitangazwa kuwa dini rasmi nchini, huku takribani asilimia 90% ni waislamu washia ukifuatiwa na  wasuni wakiwa na asilimia 10% huku dini nyingine zikiwa na asilimia chache nchini humo.

  

Iran imepita katika migogoro na majanga mbalimbali ikiwemo vita na Iraq iliyodumu kwa miaka nane na kusababisha vifo vingi, na matetemeko makubwa mawili likiwemo lile la mwaka 1990 na 2003 ambayo yote yalisababisha vifo vya watu takribani elfu arobaini.

Iran ambayo siku za hivi karibuni imekuwa na ushawishi mkubwa karibia  eneo zima la mashariki ya kati ikilinganishwa na miongo mingi iliyopita ambapo Saudi Arabia ndiyo nchi iliyokuwa na ushawishi bila upinzani thabiti kutoka Iran, kutokana na kuwa  washirika katika ukanda huo, ambapo mshirika mkubwa wa nchi hiyo ni rais Bashir-al-Assad wa Syria.

Aidha Iran  imekuwa ikishutumiwa kujihusisha na  uundaji wa silaha za nyuklia na kuchochea  ugaidi katika  mashariki ya kati na mataifa ya ulaya na imekuwa ikishutumwa na  nchi nyingine za mashariki ya kati, ambapo ivi karibuni Israel kupitia waziri mkuu wake Benjamini Netanyau  kutositisha mpango wake wa nyuklia licha ya kuingia makataba na nchi za magharibi.

Katika hatua nyingine, nchi hiyo imekuwa na mahusiano magumu na nchi za magharibi hasa Marekani ambapo mapatano yalichukua miaka hadi kufikiwa mwaka 2015,  ambapo iliingia mkataba na mataifa sita yenye ushawishi mkubwa duniani ikiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi, Ujerumani na China, ambapo makubaliano hayo  yaliirejesha kuwa imara kutokana na kuondolewa vikwazo mbalimbali ilivyokuwa imewekewa na nchi hizo.

Ivi karibuni Marekani imejiondoa katika mpango huo,  huku nchi nyingine za ulaya zikipinga uamuzi huo wa Marekani na kuwa mkataba huo ndio nafasi nzuri ya kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Uhusiano wa Marekani na Iran umekuwa wa kusuasua tangu mapinduzi ya kiislamu ambapo  uhusiano huo uliimarika kidogo baada ya kuingia makubaliano hayo kabla ya kupingwa na rais wa sasa wa marekani Donald Trump kwa kuuita mkataba huo kuwa ni uongo na usio na nia njema kwa nchi ya marekani.
  
Daima Iran imekana kuunda zana za nyuklia, na ilikubali miaka mitatu iliyopita kusitisha mpango wake wa kuunda nishati ya nyuklia ili kwa upande wake iondolewe vikwazo.