Showing posts with label MAKALA. Show all posts
Showing posts with label MAKALA. Show all posts

Friday, June 23, 2017

Mfahamu Kisoka Kiungo Haruna Niyonzima.

Mfahamu Kisoka Kiungo Haruna Niyonzima.

Image may contain: 1 person, playing a sport and outdoor
Msakataji  wa kimataifa wa kabumbu Mrwanda Haruna Niyonzima, ambae ni kioungo mchezeshaji, raia  nchini Rwanda na aliyebalikiwa kipaji cha kusakata kabumbu, na kwasasa yupo Tanzania ambapo alikuja nchini Tanzania mnamo mwaka 2011 baada ya kusajiliwa na klabu ya soka ya Dar es Salaam Young African.

Tarehe ya kuzaliwa

Alizaliwa mnamo tarehe 05, Frebrury, 1990 katika mji wa Gisenyi nchini Rwanda, ambae kwa sasa anaumri wa miaka 27. Kiungo huyu  ana urefu wa 1,67m, nafasi anayocheza ni kiungo mchezshaji ambae anacheza namba 8 dimbani, ambapo anatumia mguu wa kulia kupigia.

Historia ya kisoka
Kiungo huyu mnamo oktoba 1, 2007 alisajiliwa katika klabu ya soka ya APR FC nchini Rwanda huku akitokea katika klabu ya soka ya Rayon Sports akiwa na umri wa miaka 17 na miezi 7, lakini pia alishawahi kuchezea klabu ya soka ya Etincelles. Rasmi alianza kuchezea Timu ya Taifa ya Rwanda mnamo waka 2007.

Baada ya hapo kiungo huyu alisajiliwa katika klabu ya soka ya Tanzania Dar es Salaam Young Africans mnamo tarehe 1 July 2011 akiwa na umri wa miaka 21 na mienzi minne, ameichezea klabu ya soka ya Yanga kwa mda wa misimu sita (6) ambapo ni sawa na miaka 6.


Lakini Yanga hawataweza kuwa na mchezaji huyo katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya kushindwa kufikia muafaka ingawa walikuwa bado wanamhitaji na badala yake kiungo huyo amesajiliwa katika klabu ya soka ya Simba na kuanguka saini ya kuichezea klabu hiyo kwa muda wa misimu miwili ambapo ni sawa na miaka miwili (2).


Pata kujua yanayojiri kila siku Siasa, matukio, magazeti, makala, michezo na burudani kwa kutembelea chotamtemi.blogspot.com pia unaweza kulike facebook page bofya hapa kulike page yetu. pia unaweza kujiunga na facebook group, bofya hapa kujiunga na facebook group. pia unaweza kuifollow blog.

Sunday, June 18, 2017

IGP Simon Sirro Tazama kwa jicho la tatu mauaji kibiti, Rufiji na Mkuranga.

IGP Simon Sirro Tazama kwa jicho la tatu mauaji kibiti, Rufiji na Mkuranga.

Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa matukio ya  mauaji ya kutumia silaha mkoani Pwani katika wilaya za Kibiti, Mkuranga, na Rufiji.

Matukio haya yanashitua na kutia wasiwasi mkubwa kwa wananchi na kuibua maswali mengi kutokana na kile kinachooneka kuwa ni mwendelezo wa matukio hayo.

Tangu mwezi Aprili mwaka huu kuwekuwa na mfululizo wa mauaji ya askari, raia na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani hapo.

Ambapo askari nane (8) waliuwa kwa kupingwa  risasi wakiwa katika doria, pia watu watatu akiwemo Afisa upelelezi wa wilaya ya kibiti, Mrakibu wa Polisi Peter Kubezya ambao waliuawa kwa kupigwa risasi.

Kadhalika wengine waliouawa ni Afisa Ukaguzi wa maliasili, Peter Kitundu na mlinzi Athuman Ngambo.

Mauji mengine yaliyotokea yalimuhusisha Mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Bwana Saidi Mbwana, aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho Mbwana Ally Milandu na Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamili Ally salehe.

Pia mauaji hayo, yameendelea kushamiri na hivi karibuni viongozi wa CCM akiwemo Katibu wa chama hicho, Kata ya Bungu wilaya ya Kibiti bwana Alife Mtulia aliuawa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake, pia Mwenyekiti mstaafu wa CCM wa kijiji cha Muyuni wilaya ya kibiti bwana Idd Kirungi.

Suala la mauaji bado linaendelea kuwaacha watu midomo wazi hususani katika mkoa wa pwani ambapo viongozi na raia wamekuwa wakipoteza uhai wao kwa kupigwa risasi.

IGP Simon Sirro sasa ni wakati wa kutokomeza mauaji mkoani hapo na kuondoa hofu iliyotanda miongoni mwa wananchi wa mkoa huo.

Kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama wa raia visiishie tu kukamata lakini pia, vichungunze kwa makini sababu na kiini cha mtukio ya mauaji hayo.

Halikadhalika serikali inyooshe mkono wake kwa kuvilaani vitendo vya ugaidi na ukatili, ambavyo vinasababisha kupoteza nguvu kazi na viongozi wa taifa letu.



Monday, June 05, 2017

Watanzania tumieni fursa ya serikali kuhamia Dodoma kujikwamua kiuchumi.

Watanzania tumieni fursa ya serikali kuhamia Dodoma kujikwamua kiuchumi.

Hatimae safari ya zaidi ya miaka 40 mji wa Dodoma kuwa makao makuu yatimia makao makuu ya nchi, (Tanzania) na sasa imekuwa makao makuu ya serikali ya Tanzania. Dodoma sasa yakamilika kuwa makao makuu.

Ambapo awali makao makuu ya nchi yalikuwa katika jiji la Dar es salaam lakini badae, yalihamishiwa na kupelekwa katika mji wa Dodoma huku makao makuu ya serikali yalibaki kuwa katika jiji la Dar es salaam.  Dodoma ndio mji uliuochaguliwa kuwa mji mkuu wa Tanzania kwa sababu ndi mji pekee uliopo katikati mwa Tanzania,

Baada ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambae aliamuru mpaka kufikia mwaka 2020 serikali itakuwa tayari imekwisha hamia Dodoma. Watanzania watakiwa kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi na kuondokana na janga la umasikini.

Watanzania watumie fursa hiyo kwa ujenzi wa hoteli mbalimbali za kisasa, ujenzi wa nyumba nzuri za kupangisha lakini pia wafanyabiashara na wawezekaji kubuni miradi mbalimbali ya kibiashara kutokana na mji kupanuka na ongezeko la watu ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Hali kadhalika kwa vijana wengi walioko mtaani kwa kukosa ajira, nao watumie fursa hii kujiajiri kuwa wabunifu na kujituma kwa moyo wa dhati katika shughuli mbalimbali zitakazo fanywa katika upanuzi wa mji na ujenzi wa miondo mbinu mkoani hapo.

Kutokana na ongezeko la watu na kupanuka kwa mji wawezekaji watumie fursa hiyo kwa kuongeza vyombo vya usafirishaji kama vile magari bajaji na pikipiki.

Serikali kuhamia Dodoma sasa ni fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji na kwa vijana wasio na ajira. 

Saturday, January 28, 2017

WAJUE WAGOGO MILA NA DESTURI ZAO

WAJUE WAGOGO MILA NA DESTURI ZAO

Image result for picha za wagogo
aina ya mchezo wa asili wa kabila la kigogo ukichezwa na kikundi cha ngoma za asili za kabila la kigigo


Tanzania ni moja kati  ya nchi zinazopatikana Afrika mashariki,  nchi hii  inakadiriwa kuwa na makabila zaidi ya 120, na makabila hayo ni kama  vile  wagogo, wahehe, wachanga nakadhalika. wagogo ni miongoni mwa makabila nchini, lakini kabila hili hupatikana kanda ya kati mkoa wa Dodoma.


Kabla ya ukoloni kuja nchini kabila hili lilikuwa na utawala wa jadi liliongozwa na viongozi mbalimbali almaarufu kama mtemi. Na kiongozi wa mwisho kuongoza kabila hili alikuwa ni mtemi mazengo ambaye alitoka katika kijiji cha mvumi wilaya ya Dodoma mjini.


Kabila hili limekuwa la kipekee nchini kwa kujenga nyumba za asili za kipekee, nyumba hizi huitwa

‘itembe’ ambazo hujengwa kwa fito. fito hizo hupishana pishana ili kuzuia mwanga na maji kuingia ndani, pia  huekezwa kwa udongo ambao hushikiliwa na miti midogo midogo  iitwayo walo.
nyumba za wagogo za asili. ( itembe)



Kabila hili ni miongoni mwa makabila nchini ambayo shughuli yao kuu ya kiuchumi ni kilimo na ufugaji ambapo huwasaidia katika chakula,

Mazao mabayo hulimwa zaidi na wagogo ni mazao ya chakula kama vile mtama, mahindi, karanga, njugu mawe, lakini pia mazao ya biashara ni kama vile zabibu, ufuta na alizeti ambazo

husaidia katika kuingiza kipato. 


Wagogo hula ugali wa mtama, uwele kama chakula chao kikuu, lakin pia hula  ugali wa mahindi, nyama ya ng`ombe, maziwa, mafuta ya ng`ombe, mlenda,majani ya kunde, (safwe), nakadhalika. Kabila hili linatumia silaha za jadi kwa kujilinda kama vile upinde, mshalee, mkuki, na hengo.


Hata hivyo kabila hili  lina utamaduni ambao ni wa kujivunia nchini na afrika na duniani kote, moja ya michezo ya asili katika kabila hili ni ngoma, ngoma ni mchezo ambao  wa kitamaduni zaidi katika makabila mengi Tanzania.


Ngoma  hizi ni sehemu ya utamaduni wa  mgogo lakini pia katika nchi hi ni sehem ya kujivunia kwa kuwa inasaidia kukuza na kueneza utamaduni wa mwafrika kupitia maonesho mbalimbali ya utamaduni nchini, kama vile maonesho katika makumbusho ya taifaa.





Wednesday, November 16, 2016

MORROCO NA UMOJA WA AFRICA AU.

MORROCO NA UMOJA WA AFRICA AU.

Image result for picha za ramani ya morocco
Morocco ni miongoni mwa nchi za kiafrika ambayo inapatikana kaskazini mwa bara la Afrika ambapo mji wake mkuu ni mji wa Marrakesh, ikiwa inapakana na bahari ya Atlantic  na mediterania na milima ya rugged, pia Morocco inapakana na nchi ya Algeria, Spain na magharibi mwa jagwa la Sahara.

Raia wengi wa Morocco ni raia wenye asili ya kiarabu na wanaotumia kiarabu kama lugha yao ya mawasiliano

Taifa la morroco lilikuwa chini ya taifa la ufarasa mnamo mwaka 1912 hadi mwaka 1956 mara baada ya sultani Mohamed kuwa mfalme wa taifa hilo mnamo mwaka 1957, baadae mfalme mohamed alifariki dunia mnamo mwaka 1961 na badala yake mototo wake Hasani wa pili alishika madaraka ambapo aliongoza kwa miaka 34.

baada ya marehemu mfalme Mohamed Hasani wa pili ambae alikuwa  baba wa mfalme wa sita, Morocco ilianza kuwa chini ya mfalme Mohamed wa sita mnamo mwaka 1999 ambapo alianzisha mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini Morocco.

Mohamed wa sita alianzisha sera ya marekebisho ambayo ilijulikana kama Mudawana sharia ambayo ilitoa kipaumbele sana kwa wanawake.

Mnamo mwaka 2010 nchini morocco kulianzishwa katiba mpya ya nchi ikielezea mamlaka ya waziri mkuu na bunge na kumvalisha jukumu la kuwa mkuu wa kila idara serikalini.

Ikumbukwe kuwa, mnamo mwaka 1984, Morocco kupitia Mfalme Hassan II, babake mfalme wa sasa, iliamua kujiondoa katika umoja huo wakati huo ukifahamika kama Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU), kufuatia uamuzi wa umoja huo wa kuafiki uanachama wa Jamhuri ya Sahara Magharibi iliyojitangaza kuwa huru, licha ya serikali ya Rabat kuihesabu kuwa sehemu ya ardhi yake.

falme Mohammed wa VI wa Morocco ametangaza wazi azma ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika ya kutaka kurejea katika Umoja wa Afrika AU, baada ya kuondoka katika umoja huo zaidi ya miongo mitatu iliyopita.

Mfalme huyo amewatumia ujumbe viongozi wa Kiafrika walioshiriki mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika Kigali, mji mkuu wa Rwanda na kusema wakati umefika kwa nchi hiyo ya Kiarabu kurejea katika nafasi yake kwenye umoja huo. Mfalme Mohammed VI wa Morocco aliwaambia viongozi wa AU katika ujumbe huo kuwa, ingawaje Morocco iliondoka AU, lakini haikuondoka barani Afrika. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Salahuddine Mezouar hivi karibuni amekuwa katika safari za kidiplomasia katika nchi kadhaa za Kiafrika zikiwemo Misri, Libya, Sudan, Senegal, Tunisia, Cameroon, Cote D'ivoire na Ethiopia ili kuzitaarifu kuhusu uamuzi huo wa Rabat.

Kwa mara ya kwanza kihistoria Tanzania ilimpokea   mfalme Mohamed wa sita wa Morocco akitokea nchini Rwanda kuja nchini Tanzania kufanya ziara ambayo ilianza toka jumapili tarehe 23 mpaka tarehe 25 juma la nne katika wiki.

Aidha, ziara ya mfalme huyo, mbali na kujikita katika kujenga diplomasia ya nchi hizo mbili, ilitumika pia kuiomba Tanzania kusaidia kupokewa kwa Morocco katika Umoja wa Nchi za Afrika (AU).

Hii ndio morocco nchi inayokaliwa na watu wenye asli ya kiarabu.
Imeandikwa na 
Japhet japhet
email: japhetjaphet1993@gmail.com




.