Saturday, May 19, 2018

SIMULIZI ZINAISHI PRODUCTION YATANGAZA NEEMA KWA VIJANA TANZANIA


katikati ni Msemaji Mkuu wa Simulizi Zinaishi Bw. Omary Zongo akiwahamasisha wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari TSJ Dar es salaam kutumia fursa hiyo 

Taasisi inayojihusisha na masuala ya Sanaa za maandishi na uigizaji , iitwayo SIMULIZI ZINAISHI imetembelea Chuo cha uandishi wa Habari cha TIMES SCHOOL OF JOURNALISM (TSJ) kuwahimiza wanafunzi wa chuo hicho wawanie fursa ya kusimulia Moja ya simulizi iliyozalishwa na Taasisi hiyo iitwao Mungu, Mama ‘Angu.

Akiwaeleza kuhusu Fursa hiyo Msemaji wa SIMULIZIZINAISHI tz, Omar Zongo alisema, ni nafasi kwa vijana kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu, ili kujiweka katika nafasi ya ushiriki wa mashindano hayo, yatakayowatafuta vijana watakaokuwa na sifa zakuisimulia Riwaya hiyo , inayotarajiwa kurushwa katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini.

‘’Tumeona ni nafasi nzuri kuwaletea fursa hii, ili kuleta chachu ya ushindani kutoka kwa vijana mbalimbali wenye vipaji waliopo vyuoni, tayari tumeshaanza kuwafahamisha wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari namawasiliano kwa uma, tukaona si vibaya kama tukifika na hapa chuoni kwenu ili kuwapa nafasi hii ya pekee.” Alieleza Zongo.

Wakati wa utambulisho wa Mradi huo unaosimamiwa na timu ya vijana wajasiriamali, ambao pia ni wanahabari, Mratibu mkuu wa Mradi huo Bwana Charles Kombe, ameelezea namna ambavyo wameona umuhimu wa vijana kukutana kutoka katika maeneo tofauti, ili kuleta nafasi yakujuana nakupena fursa mbalimbali za ajira.

“nafikiri hii ni nafasi nzuri sana kwa ninyi kuchukua fomu kwa wingi, ili muweze kukutana na vijana wenzenu wengi wenye ‘visioni’ kubwa, nadhani mtabadilishana mawazo na itakuwa njia nzuri ya kujenga mahusiano mazuri hata kwa baadae” Amesisitiza Kombe.

Awali akiwahimiza wanafunzi wa chuo hicho wajitokeze kwa wingi kununua fomu, mshauri wa wanafunzi kutoka chuo hicho, ambaye pia ni mwaimu wa nidhamu Sir Georg, amewataka wanafunzi kutopuuzia fursa hiyo, kwa kuwa ni moja ya njia yakujiweka katika soko la ajira nakujitangaza.

Mradi huo tayari umeshaanza rasmi na unatarajiwa kuwashindanisha wanafunzi zaidi ya mia moja kutoka mikoa yote Tanzania, ambao kwa hivi sasa tayari muamko umekuwa mkubwa na zoezi likitarajiwa kukamilika mapema mwezi wa saba mwaka huu kwa kuwatangaza washindi watakaobahatika kuisimulia Riwaya hiyo ya MUNGU, MAMA ANGU.

Fomu za ushiriki zinapatikana kwa mawasiliano ya namba za simu 0652721612, 0788777658 Au 0677303582, Kwa njia ya barua pepe ni simulizizinaishi@gmail.com .




SHARE THIS

1 comment:

  1. Kazi, nzuri sana, nafarijika kuona vijana mnaamka,Resul never lie

    ReplyDelete

Comment hapa