Saturday, January 28, 2017

WAJUE WAGOGO MILA NA DESTURI ZAO

Image result for picha za wagogo
aina ya mchezo wa asili wa kabila la kigogo ukichezwa na kikundi cha ngoma za asili za kabila la kigigo


Tanzania ni moja kati  ya nchi zinazopatikana Afrika mashariki,  nchi hii  inakadiriwa kuwa na makabila zaidi ya 120, na makabila hayo ni kama  vile  wagogo, wahehe, wachanga nakadhalika. wagogo ni miongoni mwa makabila nchini, lakini kabila hili hupatikana kanda ya kati mkoa wa Dodoma.


Kabla ya ukoloni kuja nchini kabila hili lilikuwa na utawala wa jadi liliongozwa na viongozi mbalimbali almaarufu kama mtemi. Na kiongozi wa mwisho kuongoza kabila hili alikuwa ni mtemi mazengo ambaye alitoka katika kijiji cha mvumi wilaya ya Dodoma mjini.


Kabila hili limekuwa la kipekee nchini kwa kujenga nyumba za asili za kipekee, nyumba hizi huitwa

‘itembe’ ambazo hujengwa kwa fito. fito hizo hupishana pishana ili kuzuia mwanga na maji kuingia ndani, pia  huekezwa kwa udongo ambao hushikiliwa na miti midogo midogo  iitwayo walo.
nyumba za wagogo za asili. ( itembe)



Kabila hili ni miongoni mwa makabila nchini ambayo shughuli yao kuu ya kiuchumi ni kilimo na ufugaji ambapo huwasaidia katika chakula,

Mazao mabayo hulimwa zaidi na wagogo ni mazao ya chakula kama vile mtama, mahindi, karanga, njugu mawe, lakini pia mazao ya biashara ni kama vile zabibu, ufuta na alizeti ambazo

husaidia katika kuingiza kipato. 


Wagogo hula ugali wa mtama, uwele kama chakula chao kikuu, lakin pia hula  ugali wa mahindi, nyama ya ng`ombe, maziwa, mafuta ya ng`ombe, mlenda,majani ya kunde, (safwe), nakadhalika. Kabila hili linatumia silaha za jadi kwa kujilinda kama vile upinde, mshalee, mkuki, na hengo.


Hata hivyo kabila hili  lina utamaduni ambao ni wa kujivunia nchini na afrika na duniani kote, moja ya michezo ya asili katika kabila hili ni ngoma, ngoma ni mchezo ambao  wa kitamaduni zaidi katika makabila mengi Tanzania.


Ngoma  hizi ni sehemu ya utamaduni wa  mgogo lakini pia katika nchi hi ni sehem ya kujivunia kwa kuwa inasaidia kukuza na kueneza utamaduni wa mwafrika kupitia maonesho mbalimbali ya utamaduni nchini, kama vile maonesho katika makumbusho ya taifaa.






SHARE THIS

1 comment:

Comment hapa