
Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam wamefunguka mengi kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wa Marekani, kuwa watanzania waige mfano kutoka kwa aliyekuwa mgombea uraisi wa chama cha democratic Bi Hillary Clinton kwa kukubaliana na matokeo na si kufanya migomo na maandamano.
Wanafunzi hao wamesema, '' watanzania au siasa ya Tanzania tunatakiwa kuiga mazuri kutoka uchaguzi uliofanyika marekani tujifunze kuwa na moyo wa subira au uvumilivu wa kisiasa kama ilivyokuwa Bi Hillary Clinton kukubaliana na matokeo ya uchaguzi mpaka kumpigia simu mpinzani wake Donald Trump na kumpongeza kwa ushindi wake.''
Hata hivyo mbali na Donald Trump kuonekana kuwa na kashfa mbaya ya maneno yake aliyoyatamka wakati wa kampeni zake za uraisi na watu kuamini kuwa trump hataweza kushinda uchaguzi huo, ''watu wengi waliamini Trump hatashinda kiti cha uraisi kutokana na maneno yake aliyoyasema katika kapen zake'',Mateso Warioba mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo kikuu cha Dar es salaam.
.
0 comments:
Comment hapa