Yanga Yatoa sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya City.
leo kumerindima mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara VPL, mchezo ambao umepigwa katika dimba la sokoine jijini Mbeya, nyasi za dimba hilo zimeikutanisha timu ya soka ya Yanga ambao wamechuana vikali na wagonga nyundo wa mbeya, Mbeya City
katika mchezo huo Yanga wamekubali sare ya bao 1-1 bao la Yanga lilipatikakana kunako dakika ya 57 ya kipindi cha pili kupitia mchezaji Raphaeli Daudi kwa mpira wa adhabu uliopigwa kama krosi na mchezaji Juma Abdul,
mchezo uliendelea huku mbeya city wakitafuta bao la kusawazisha kwa udi na uvumba na jitihada zao zilionesha kuzaa matunda kunako dakika ya 90 kupitia mchezaji Idd Nado ambae aliisawazishia timu yake na kubadili matokeo kuwa 1-1.
hivyo kutokana na matokeo hayo Yanga inakuwa na jumla ya alama 48 ikiendelea kuwa nafasi ya pili ikiwa na jumla ya michezo 23 huku Mbeya city ikiwa na jumla ya alama 27 ikiwa nafasi ya 10 na jumla ya michezo 25
Endelea kufatilia chotamtemi blog kwa habari za michezo siasa kitaifa na kimataifa
0 comments:
Comment hapa