Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Sunday, February 03, 2019

Simba SC Yaburuzwa Bao 5-0 Dhidi ya  Al Ahly

Simba SC Yaburuzwa Bao 5-0 Dhidi ya Al Ahly



Katika michezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika,  katika kundi D jana ndani mji wa Alexandria Misri kulipigwa mtanange mkali uliozikutanisha timu ya Simba SC ambao walikuwa ugenini kuchuana na Al Ahly.

katika dakika 90 za mchezo huo Simba iliweza kuruhusu alama tatu kwenda kwa timu ya Al Ahly baada ya kukubali kichapo cha bao 5- 0, ambapo magoli yote yalifungwa ndani ya kipindi cha kwanza.

kikosi cha simba kimekuwa na mwendelezo wa kufungwa bao tano kwa sifuru baada ya kupigwa na AS Vita nchini Congo, Simba inaendelea kushika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kundi D ikiwa na jumla ya alama 3 huku Al Ahly ikizidi kujiimarisha kileleni ikiwa na jumla ya alama 7 huku As Vita ikishika nafasi ya pili baada ya jana kutoa sare ya mabao 2- 2 na JS Saoura, na kuifanya JS Saoura iendelea kuburuza mkia katika kundi hilo .

Friday, February 01, 2019

Mechi Zitakazochenzwa Leo  Ligi Kuu Bara, TPL

Mechi Zitakazochenzwa Leo Ligi Kuu Bara, TPL

Related imageLeo kutalindima michezo minne ya ligi kuu Tanzania bara ambayo itahusisha timu   timu nane zitakazo chuana  kwenye viwanja vinne kutafuta pointi tatu ikiwa ni mzunguko wa pili.

Kagera Sugar watacheza  na kikosi cha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, KMC wapo mkoani Shinyanga watacheza na Stand United uwanja wa Kambarage.


JKT Tanzania wataikaribisha Mwadui uwanja wa Isamuhyo na Ruvu Shooting leo atakuwa kazini kumenyana na Mbeya City uwanja wa Mabatini.

Thursday, June 14, 2018

 Urusi Vs Saudi Arabia, Kufungua kombe La Dunia Leo

Urusi Vs Saudi Arabia, Kufungua kombe La Dunia Leo

Related image

Michuano ya Kombe la Dunia ya Fifa ya mwaka 2018 inaanza leo nchini Urusi ambapo Urusi watacheza dhidi ya Saudi Arabia baada ya kufanyika kwa sherehe ya ufunguzi katika uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow. Mechi hiyo itaanza saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki.

Michuano hiyo itashirikisha mataifa 32, wakiwemo mabingwa watetezi Ujerumani, na itakuwa na mechi 64 zitakazochezwa katika kipindi cha siku 32.

Fainali itachezwa 15 Julai.Fainali za sasa za Kombe la Dunia ambazo ni za 21 zitachezwa katika viwanja 12 katika miji 11 nchini Urusi, ambayo inapatikana eneo la upana wa maili zaidi 1,800.

Kutokana na hili, kutakuwa na tofauti kubwa katika wakati mechi zinachezwa.  Ujerumani, waliowashinda Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia 2014, wanapania kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mtawalia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1962

Tuesday, June 12, 2018

Orodha Kamili ya washindi wa tuzo za Mo Simba Awards 2018

Orodha Kamili ya washindi wa tuzo za Mo Simba Awards 2018


Jana Jumatatu usiku  mdhamini mkuu wa Mabingwa wa Ligi Kuu Bara klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji aliandaa tuzo maalum ‘Mo Simba Awards 2018’ zilizofanyika Hyatt Regency jijini Dar es salaam kwaajili ya kuwapongeza wachezaji wa klabu hiyo waliofanya vizuri mwaka huu.


WASHINDI WA TUZO ZA MO SIMBA 2018

1.   GOLIKIPA BORA WA MWAKA
A.  Aishi Manula - WINNER
B.  Said Mohamed 'Nduda'
C.   Emmanuel Elias Mseja

2.   BEKI BORA WA MWAKA
A.  Yusuph Mlipili
B.  Erasto Nyoni - WINNER
C.  Shomari Kapombe

3.   KIUNGO BORA WA MWAKA
A.  Jonas Mkude
B.  James Kotei
C.  Shiza Kichuya – WINNER

4.   MSHAMBULIAJI BORA WA MWAKA
A.  Emmanuel Okwi - WINNER
B.  John Bocco
C.  Shiza Kichuya

5.   MCHEZAJI BORA MWANAMKE WA MWAKA
A.  Rukhia Salum
B.  Zainabu Rashidi Pazzi - WINNER
C.  Dotto Makunja

6.   MCHEZAJI BORA MDOGO WA MWAKA
A.  Ally Salim (GK)
B.  Rashid Juma – WINNER
C.  Salumu Shabani

7.   GOLI BORA LA MWAKA
-      John Bocco (Simba VS Mwadui)

8.   TUZO YA BENCHI LA UFUNDI
A.  Pierre Lechantre – Kocha Mkuu
B.  Masoud Djuma – Kocha Msaidizi
C.  Mohamed Aymen – Kocha wa Viungo
D.  Muharam Mohamed – Kipa wa Makipa
E.  Richard Robert – Meneja wa Timu
F.   Yassin Gembe – Daktari wa Timu
G.  Abbas Selemani – Mratibu

9. SHABIKI BORA WA MWAKA
- Fihi Salehe Kambi

10. MHAMASISHAJI BORA WA MWAKA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
A.  Hamis Mwinjuma (Mwana FA) - WINNER
B.  Salama Jabir – WINNER
C.  Zitto Kabwe
D.  Vyonne Cherrie (Monalisa)
E.  Omary Nyembo (Ommy Dimpoz)

11. MHAMASISHAJI BORA
- Haji Manara

12. TAWI BORA LA MWAKA
A.  Wazo Hill
B.  Ubungo Terminal - WINNER
C.  Vuvuzela

13. KIONGOZI BORA WA MWAKA
          - Kaimu Rais wa klabu ya Simba, Salim Abdallah Muhene

14. TUZO YA WASIMAMIZI WA MCHAKATO WA MABADILIKO

A.  Jaji Mstaafu Thomasi Mihayo
B.  Wakili Damasi Ndumbaro
C.  Abdulrazak Badru
D.  Mussa Hassan Zungu
E.  Yusuph Nassoro
F.  Brenda Mrema
G. Mzee Hamis Boma
H.  Revocatus Cosmas Sangu
I.    Hashim Nyendage
J.   Gervas Alpha Honest
K.  Emmanuel Metusela Urembo
L.   Mulamu Nghambi
M. Selemani Omari
N.  Aziz Kifile
O. Salim Abdallah Muhene
P.  Arnold Kashembe
Q. Omari Bakari Mtika
R.  Evodius Mtawala

15. TUZO YA HESHIMA (LIFETIME ACHIEVEMENT)
        - Selemani Matola – WINNER

16. MCHEZAJI BORA WA MWAKA
A.  Emmanuel Okwi
B.  John Bocco - WINNER
C.  Shiza Kichuya




Sunday, June 10, 2018