Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Sunday, September 23, 2018

Tuesday, September 11, 2018

Nafasi Arts Space Yaja kivingine

Nafasi Arts Space Yaja kivingine



katika kusherehekea miaka kumi (10) ya kikundi cha sanaa nchini Tanzania, Nafasi Arts Space, kimekuja kivingine,  mwezi huu ambao umepewa jina la sanaa yetu, kikundi hichi kitatoa na  kutembelea vituo mbalimbali vya afya ikiwemo Hospitali ya taifa Muhimbili, lakini pia kitashiriki katika siku ya usafi Duniani tarehe 15, September mwaka huu kwa kufanya usafi katika fukwe za coco beach.

Hayo yamefahamika wakati Mkurugenzi wa sanaa hizi Bi. Rebecca Correy na wajumbe wa bodi wakizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa nafasi, ambapo amesema kuwa katika mwezi huu wa sanaa yetu kikundi hiki mbali na kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili lakini pia kutakuwa na matukio mbalimbai ya kisanaa kwa ajili ya umma, Uzinduzi wa chama cha uchoraji, kuchangisha pesa kwa njia ya mnada, uchoraji wa  ya Graffit katika stendi ya basi ya Morocco, na tarehe 29 September ndio kilele cha sherehe  hizo ambazo zitamalizikia na tamasha la muziki katika ukumbi wa nafasi.

katika kuelezea mafanikio mjumbe wa kikundi hicho Bi. Sauda Simba alisemak kuwa baada ya miaka kumi programu za nafasi zimeongezeka kwa kiasi kikubwa , mahusiano baina ya wasanii wa ndani na nje yamepanuka, kuonesha filamu ikishirikkana na kijiweni cinema,

Mbali na mafanikio hayo Bi. Sauda Simba aliongeza kwa kusema changamoto zinazowakabili ikiwemo na kukosa sehemu rasmi inayomilikiwa na kikundi hicho kwa ajili ya shuguli zao, aliongeza kwa kusema kuwa sehemu iliyopo ni ya kupangisha hivyo inakuwa ni gharama katika uendeshaji wa shughuli zao.

kwa upande wa msanii katika kituo hicho Bw. Musa Sango alisema kuwa amefaidika kupitia nafasi kwa kukutana na wasanii wakubwaa wa nje na kubadilishana nao mawazo na kukuza kipaji cha sanaaa za uchoraji, na kutoa wito kwa jamii kutembelea ofisi za nafasi kwa ajili ya kujifunza na kununua sanaaa ambazo zinatengenezwa na watanzania.

Nafasi arts Space ilianzishwa mnamo mwaka 2008 kwa kikundi kidogo cha wasanii wa Tanzania, kwa ajili ya wasanii nchini kuwa sehemu yao ya kufanyia kazi zao, pamoja na msaada kutoka ubalozi wa Denmark.
Ratiba ya matukio yote ya Nafasi Arts Space katika kusherehekea miaka kumi (10) ya kikundi hicho
 

Thursday, June 07, 2018

 TANZIA: Sam Wa Ukweli Afariki Dunia

TANZIA: Sam Wa Ukweli Afariki Dunia


 Msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu

mwili wake kupelekwa katika hospital ya Mwananyamala huku Producer wake Steve aliekua akifanya kazi na Msanii huyo amesema Sam alikuwa akiumwa na walipomuuliza alisema ni UKIMWI wa kulogwa.
credit Millard Ayo

Tutaendelea kukujuza yanayojirir zaidi



Monday, May 28, 2018

‘Hedhi si jambo la aibu jamii ishiriki katika kuhakikisha hedhi salama’,  wadau wa jinsia.

‘Hedhi si jambo la aibu jamii ishiriki katika kuhakikisha hedhi salama’, wadau wa jinsia.



Tanzania inaungana na nchi nyingine kuadhimisha siku ya hedhi duniani huku wadau mbalimbali wa masuala ya jinsia wakiendelea kulalamikia ushiriki wa jamii katika masuala ya hedhi na kuwa hedhi imekuwa ikichukuliwa kama jambo la siri ambalo halipaswi kuzungumziwa kwa wazi katika jamii.

Agness Lukanga ni mmoja wa wajumbe wa mtandao wa jinsia nchini (TNGP) amesema kuwa jamii imekuwa ikiwaachia suala hili watoto wa kike jambo linalowafanya wakose amani na kujiamini wakiwa katika siku zao.
 Ameendelea kwa kusema kuwa watoto wa kike wanatakiwa kuhakikishiwa na kuandaliwa mazingira ya kuweza kufurahia hedhi  na kuiona kama  sehemu ya  uumbaji ambayo huwatengeneza wao kuwa Wanawake kamili na kuwa mama wa baadaye.

Aidha,  Jackson Malangalila ambaye pia ni mjumbe wa mtandao huo wa kijinsia  amesema kuwa wanaume wamekuwa nyuma katika kuhakikisha hedhi salama na kuliona jambo hilo kama suiala la aibu ambalo hawapaswi kushirikishwa  na kusema kuwa ushiriki wao wa moja kwa moja utamfanya mtoto wa kike kuwa  huru kueleza matatizo anayokumbana nayo wakati wa hedhi kama vile kupata maumivu ya tumbo.

Ripoti zinaonyesha asilimia 65 ya wanawake na wasichana nchini hawamudu kupata ‘pedi’ wakati wa siku zao za hedhi,  huku kauli mbiu ya mwaka ikiwa inasema kuwa  ‘hakuna tena vikwazo’.

Pia wamesisitiza kuwa serikali kupitia halmashauri zake inapaswa kuhusika moja kwa moja kumsaidia mtoto wa kike kupita katika siku zake akijisikia furaha na salama,  ikiwemo kuziondolea kabisa  kodi taulo hizo za kike maarufu kama pedi,  na kufanyikisha upatikanaji wake kuwa rais na wa gharama nafuu ama bure kabisa.

Maadhimisho hayo yanafanyika leo mbwalo la maofisa wa polisi , huku Mgeni rasmi wa akiwa ni Faustine Ndugulile,  Naibu waziri wa afya,  ambapo kutakuwa na ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi 500 wa shule za msingi na sekondari  jijini Dar-es-salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari  jana, mkurugenzi wa Asasi ya chief of promotions, Amon Mkoga alisema kuwa zaidi ya Wasichana  850,000 wanakosa wiki sita za masomo kila mwaka huku Wanawake wakipoteza saa zao za kufanya kazi.