Tanzania
inaungana na nchi nyingine kuadhimisha siku ya hedhi duniani huku wadau
mbalimbali wa masuala ya jinsia wakiendelea kulalamikia ushiriki wa jamii
katika masuala ya hedhi na kuwa hedhi imekuwa ikichukuliwa kama jambo la siri
ambalo halipaswi kuzungumziwa kwa wazi katika jamii.
Agness
Lukanga ni mmoja wa wajumbe wa mtandao wa jinsia nchini (TNGP) amesema kuwa
jamii imekuwa ikiwaachia suala hili watoto wa kike jambo linalowafanya wakose
amani na kujiamini wakiwa katika siku zao.
Ameendelea kwa kusema kuwa watoto wa kike
wanatakiwa kuhakikishiwa na kuandaliwa mazingira ya kuweza kufurahia hedhi na kuiona kama sehemu ya uumbaji ambayo huwatengeneza wao kuwa Wanawake
kamili na kuwa mama wa baadaye.
Aidha,
Jackson Malangalila ambaye pia ni mjumbe
wa mtandao huo wa kijinsia amesema kuwa
wanaume wamekuwa nyuma katika kuhakikisha hedhi salama na kuliona jambo hilo
kama suiala la aibu ambalo hawapaswi kushirikishwa na kusema kuwa ushiriki wao wa moja kwa moja utamfanya
mtoto wa kike kuwa huru kueleza matatizo
anayokumbana nayo wakati wa hedhi kama vile kupata maumivu ya tumbo.
Ripoti
zinaonyesha asilimia 65 ya wanawake na wasichana nchini hawamudu kupata ‘pedi’
wakati wa siku zao za hedhi, huku kauli
mbiu ya mwaka ikiwa inasema kuwa ‘hakuna
tena vikwazo’.
Pia
wamesisitiza kuwa serikali kupitia halmashauri zake inapaswa kuhusika moja kwa
moja kumsaidia mtoto wa kike kupita katika siku zake akijisikia furaha na salama,
ikiwemo kuziondolea kabisa kodi taulo hizo za kike maarufu kama pedi, na kufanyikisha upatikanaji wake kuwa rais na
wa gharama nafuu ama bure kabisa.
Maadhimisho
hayo yanafanyika leo mbwalo la maofisa wa polisi , huku Mgeni rasmi wa akiwa ni
Faustine Ndugulile, Naibu waziri wa afya,
ambapo kutakuwa na ugawaji wa taulo za
kike kwa wanafunzi 500 wa shule za msingi na sekondari jijini Dar-es-salaam.
Akizungumza
na vyombo vya habari jana, mkurugenzi wa Asasi
ya chief of promotions, Amon Mkoga alisema kuwa zaidi ya Wasichana 850,000 wanakosa wiki sita za masomo kila
mwaka huku Wanawake wakipoteza saa zao za kufanya kazi.
0 comments:
Comment hapa