Iran ni moja kati ya nchi takribani 17 zinazopatikana
mashariki ya kati, inayoundwa na sehemu kubwa ya Asia ya magharibi pamoja na
Afrika ya Kasikazini, huku Teheran ukiwa ndio mji mkuu wa nchi hiyo na lugha rasmi ni lugha ya kiajemi
(Farsi).
Irani imekuwa huru tangu kutokea mapinduzi ya kiislamu
mwaka 1979 yaliyoangusha utawala wa kifalme, jina Irani lilichukuliwa kuwa jina rasmi la nchi
hiyo badala ya Persia, kabla ya kuwa jamhuri ya kiislamu ya Irani
baada ya mapinduzi ama Uajemi jina ambalo
limejulikana tangu kale.
Mamlaka kuu ya nchi hiyo iko mikononi mwa kiongozi
mkuu wa mapinduzi ambaye huchaguliwa na mkutano wa wataalamu wa uongozi kwa
muda wa maisha yake, anayesimamia siasa ya nchi kwa jumla, aidha kiongozi huyo
ana mamlaka ya kuweza kumwachisha urais rais wa nchi hiyo, ambapo Ayatollah
Khamenei ni kiongozi wa pili tangu mapinduzi ya kiislamu.
Serikali inayoongozwa na rais wa Uajemi ambaye ana
nafasi ya pili baada ya kiongozi mkuu. Huchaguliwa na wananchi wote kwa kipindi cha miaka minne na anaweza
kuchaguliwa tena, aidha rais anaongoza serikali na kazi yake akiwa chini ya
kiongozi mkuu.
Baada ya mapinduzi uislamu wa kishia ulitangazwa kuwa dini rasmi nchini, huku
takribani asilimia 90% ni waislamu washia ukifuatiwa na wasuni wakiwa na asilimia 10% huku dini
nyingine zikiwa na asilimia chache nchini humo.
Iran imepita katika migogoro na majanga mbalimbali ikiwemo
vita na Iraq iliyodumu kwa miaka nane na kusababisha vifo vingi, na matetemeko
makubwa mawili likiwemo lile la mwaka 1990 na 2003 ambayo yote yalisababisha
vifo vya watu takribani elfu arobaini.
Iran ambayo siku za hivi karibuni imekuwa na ushawishi mkubwa karibia eneo zima la mashariki ya kati ikilinganishwa
na miongo mingi iliyopita ambapo Saudi Arabia ndiyo nchi iliyokuwa na ushawishi
bila upinzani thabiti kutoka Iran, kutokana na kuwa washirika
katika ukanda huo, ambapo mshirika mkubwa wa nchi hiyo ni rais Bashir-al-Assad wa Syria.
Aidha Iran imekuwa
ikishutumiwa kujihusisha na uundaji wa
silaha za nyuklia na kuchochea ugaidi
katika mashariki ya kati na mataifa ya
ulaya na imekuwa
ikishutumwa na nchi nyingine za
mashariki ya kati, ambapo ivi karibuni Israel kupitia waziri mkuu wake
Benjamini Netanyau kutositisha mpango wake wa nyuklia licha ya kuingia makataba na nchi za magharibi.
Katika hatua nyingine, nchi hiyo imekuwa na mahusiano magumu
na nchi za magharibi hasa Marekani ambapo mapatano yalichukua miaka hadi
kufikiwa mwaka 2015, ambapo iliingia
mkataba na mataifa sita yenye ushawishi mkubwa duniani ikiwemo Marekani, Uingereza,
Ufaransa, Urusi, Ujerumani na China, ambapo makubaliano hayo yaliirejesha kuwa imara kutokana na kuondolewa
vikwazo mbalimbali ilivyokuwa imewekewa na nchi hizo.
Ivi karibuni Marekani imejiondoa katika mpango huo, huku nchi nyingine za ulaya zikipinga uamuzi huo
wa Marekani na kuwa mkataba huo ndio nafasi nzuri ya kuizuia Iran kutengeneza
silaha za nyuklia.
Uhusiano wa Marekani na Iran umekuwa wa kusuasua tangu mapinduzi
ya kiislamu ambapo uhusiano huo
uliimarika kidogo baada ya kuingia makubaliano hayo kabla ya kupingwa na rais
wa sasa wa marekani Donald Trump kwa kuuita mkataba huo kuwa ni uongo na usio
na nia njema kwa nchi ya marekani.
Daima Iran imekana kuunda zana za nyuklia, na ilikubali
miaka mitatu iliyopita kusitisha mpango wake wa kuunda nishati ya nyuklia ili
kwa upande wake iondolewe vikwazo.
0 comments:
Comment hapa