Tuesday, September 11, 2018

Nafasi Arts Space Yaja kivingine



katika kusherehekea miaka kumi (10) ya kikundi cha sanaa nchini Tanzania, Nafasi Arts Space, kimekuja kivingine,  mwezi huu ambao umepewa jina la sanaa yetu, kikundi hichi kitatoa na  kutembelea vituo mbalimbali vya afya ikiwemo Hospitali ya taifa Muhimbili, lakini pia kitashiriki katika siku ya usafi Duniani tarehe 15, September mwaka huu kwa kufanya usafi katika fukwe za coco beach.

Hayo yamefahamika wakati Mkurugenzi wa sanaa hizi Bi. Rebecca Correy na wajumbe wa bodi wakizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa nafasi, ambapo amesema kuwa katika mwezi huu wa sanaa yetu kikundi hiki mbali na kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili lakini pia kutakuwa na matukio mbalimbai ya kisanaa kwa ajili ya umma, Uzinduzi wa chama cha uchoraji, kuchangisha pesa kwa njia ya mnada, uchoraji wa  ya Graffit katika stendi ya basi ya Morocco, na tarehe 29 September ndio kilele cha sherehe  hizo ambazo zitamalizikia na tamasha la muziki katika ukumbi wa nafasi.

katika kuelezea mafanikio mjumbe wa kikundi hicho Bi. Sauda Simba alisemak kuwa baada ya miaka kumi programu za nafasi zimeongezeka kwa kiasi kikubwa , mahusiano baina ya wasanii wa ndani na nje yamepanuka, kuonesha filamu ikishirikkana na kijiweni cinema,

Mbali na mafanikio hayo Bi. Sauda Simba aliongeza kwa kusema changamoto zinazowakabili ikiwemo na kukosa sehemu rasmi inayomilikiwa na kikundi hicho kwa ajili ya shuguli zao, aliongeza kwa kusema kuwa sehemu iliyopo ni ya kupangisha hivyo inakuwa ni gharama katika uendeshaji wa shughuli zao.

kwa upande wa msanii katika kituo hicho Bw. Musa Sango alisema kuwa amefaidika kupitia nafasi kwa kukutana na wasanii wakubwaa wa nje na kubadilishana nao mawazo na kukuza kipaji cha sanaaa za uchoraji, na kutoa wito kwa jamii kutembelea ofisi za nafasi kwa ajili ya kujifunza na kununua sanaaa ambazo zinatengenezwa na watanzania.

Nafasi arts Space ilianzishwa mnamo mwaka 2008 kwa kikundi kidogo cha wasanii wa Tanzania, kwa ajili ya wasanii nchini kuwa sehemu yao ya kufanyia kazi zao, pamoja na msaada kutoka ubalozi wa Denmark.
Ratiba ya matukio yote ya Nafasi Arts Space katika kusherehekea miaka kumi (10) ya kikundi hicho
 

SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa