Msakataji wa kimataifa wa kabumbu Mrwanda Haruna
Niyonzima, ambae ni kioungo mchezeshaji, raia nchini Rwanda na aliyebalikiwa kipaji cha
kusakata kabumbu, na kwasasa yupo Tanzania ambapo alikuja nchini Tanzania
mnamo mwaka 2011 baada ya kusajiliwa na klabu ya soka ya Dar es Salaam Young
African.
Tarehe
ya kuzaliwa
Alizaliwa mnamo tarehe 05, Frebrury, 1990 katika mji
wa Gisenyi nchini Rwanda, ambae kwa sasa anaumri wa miaka 27. Kiungo huyu ana urefu wa 1,67m, nafasi anayocheza ni
kiungo mchezshaji ambae anacheza namba 8 dimbani, ambapo anatumia mguu wa kulia
kupigia.
Historia
ya kisoka
Kiungo huyu mnamo oktoba 1, 2007 alisajiliwa katika
klabu ya soka ya APR FC nchini Rwanda huku akitokea katika klabu ya soka ya
Rayon Sports akiwa na umri wa miaka 17 na miezi 7, lakini pia alishawahi
kuchezea klabu ya soka ya Etincelles. Rasmi alianza kuchezea Timu ya Taifa ya
Rwanda mnamo waka 2007.
Baada ya hapo kiungo huyu alisajiliwa katika klabu
ya soka ya Tanzania Dar es Salaam Young Africans mnamo tarehe 1 July 2011 akiwa
na umri wa miaka 21 na mienzi minne, ameichezea klabu ya soka ya Yanga kwa mda
wa misimu sita (6) ambapo ni sawa na miaka 6.
Lakini Yanga hawataweza kuwa na mchezaji huyo katika
msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya kushindwa kufikia muafaka
ingawa walikuwa bado wanamhitaji na badala yake kiungo huyo amesajiliwa katika
klabu ya soka ya Simba na kuanguka saini ya kuichezea klabu hiyo kwa muda wa
misimu miwili ambapo ni sawa na miaka miwili (2).
0 comments:
Comment hapa