Wakuu wa afya wa Nigeria wanasema idadi ya watu waliothibitishwa kufa kwa sababu ya homa ya uti wa mgongo, sasa imefikia 300.
Mlipuko wa homa hiyo sasa umetapakaa, na kua-thiri mikoa 16, kaskazini mwa nchi.
Kuna wagonjwa elfu-mbili-na-nusu wengine wanao-shu-kiwa kuwa na ugonjwa huo, ambapo nyama inayozunguka ubongo na uti wa mgongo, huvimba.
Wengi wanaoambukizwa ni watoto.
Wakuu wanaonya kuwa aina ya virusi vya mlipuko wa hivi sasa, ni tofauti, inayojulikana kama aina ya C na wakuu hawana chanjo ya kutosha kupambana nao.
Homa ya uti wa mgongo, yaani meningitis, ni nadra kutokea Nigeria, ingawa watu zaidi ya elfu mbili walikufa, katika mlipuko wa miaka minane iliyopita.
0 comments:
Comment hapa