Saturday, March 25, 2017

Jeshi la polisi mkoani Dodoma lanasaShehena ya tani 50 za ‘viroba’.

JESHI la Polisi mkoani Dodoma kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), limekamatwa shehena ya pombe kali zilizofungashwa katika mifuko ya plastiki, maarufu kama viroba, zenye uzito wa tani 50.57.
Pombe hizo zenye thamani ya Sh. milioni 354.4 zimekamatwa zimehifadhiwa kwenye makasha 3,972 ndani ya ghala la wafanyabiashara wawili wanaomiliki kampuni ya Takawedo Investment iliyoko Kisasa, manispaa ya Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, aliwataja wafanyabiashara waliokamatwa wakimiliki shehena hiyo ni Alexander Lipindo na ndugu yake William Lupindo.

Mambosasa alitaja aina ya pombe zilizokamatwa kwa wafanyabiashara hao ni konyagi katoni 1,399, Valeur katoni 712, Kiroba Original 1,782, Bismark katoni 24 na katoni 55 za Zanzi.

Alisema mpaka sasa shehena hiyo imezuiwa katika ghala hilo na kuwekewa utepe maalum wa TFDA ili isiondolewe sehemu hiyo.

Kamanda huyo alisema kutokana na kukamatwa kwa shehena hiyo, wamiliki hao hawataruhusiwa kusambaza mitaani hadi maelekezo mengine ya serikali yatakapotolewa.

"Ninawaomba wananchi waendelee kushirikiana na vyombo vya dola kuwafichua wasambazaji na watumiaji wa pombe hizi kali zilizopigwa marufuku na serikali,” alisema Mambosasa.

SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa