Hatimae
safari ya zaidi ya miaka 40 mji wa Dodoma kuwa makao makuu yatimia makao makuu
ya nchi, (Tanzania) na sasa imekuwa makao makuu ya serikali ya Tanzania. Dodoma
sasa yakamilika kuwa makao makuu.
Ambapo awali makao
makuu ya nchi yalikuwa katika jiji la Dar es salaam lakini badae, yalihamishiwa
na kupelekwa katika mji wa Dodoma huku makao makuu ya serikali yalibaki kuwa
katika jiji la Dar es salaam. Dodoma ndio mji uliuochaguliwa kuwa mji mkuu
wa Tanzania kwa sababu ndi mji pekee uliopo katikati mwa Tanzania,
Baada ya serikali ya awamu
ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambae aliamuru mpaka kufikia
mwaka 2020 serikali itakuwa tayari imekwisha hamia Dodoma. Watanzania watakiwa
kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi na kuondokana na janga la umasikini.
Watanzania watumie
fursa hiyo kwa ujenzi wa hoteli mbalimbali za kisasa, ujenzi wa nyumba nzuri za
kupangisha lakini pia wafanyabiashara na wawezekaji kubuni miradi mbalimbali ya
kibiashara kutokana na mji kupanuka na ongezeko la watu ambayo itawasaidia
kujikwamua kiuchumi.
Hali kadhalika kwa
vijana wengi walioko mtaani kwa kukosa ajira, nao watumie fursa hii kujiajiri
kuwa wabunifu na kujituma kwa moyo wa dhati katika shughuli mbalimbali zitakazo
fanywa katika upanuzi wa mji na ujenzi wa miondo mbinu mkoani hapo.
Kutokana na ongezeko la
watu na kupanuka kwa mji wawezekaji watumie fursa hiyo kwa kuongeza vyombo vya
usafirishaji kama vile magari bajaji na pikipiki.
Serikali kuhamia Dodoma sasa ni fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji na kwa vijana wasio na ajira.
0 comments:
Comment hapa