Sunday, June 18, 2017

IGP Simon Sirro Tazama kwa jicho la tatu mauaji kibiti, Rufiji na Mkuranga.

Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa matukio ya  mauaji ya kutumia silaha mkoani Pwani katika wilaya za Kibiti, Mkuranga, na Rufiji.

Matukio haya yanashitua na kutia wasiwasi mkubwa kwa wananchi na kuibua maswali mengi kutokana na kile kinachooneka kuwa ni mwendelezo wa matukio hayo.

Tangu mwezi Aprili mwaka huu kuwekuwa na mfululizo wa mauaji ya askari, raia na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani hapo.

Ambapo askari nane (8) waliuwa kwa kupingwa  risasi wakiwa katika doria, pia watu watatu akiwemo Afisa upelelezi wa wilaya ya kibiti, Mrakibu wa Polisi Peter Kubezya ambao waliuawa kwa kupigwa risasi.

Kadhalika wengine waliouawa ni Afisa Ukaguzi wa maliasili, Peter Kitundu na mlinzi Athuman Ngambo.

Mauji mengine yaliyotokea yalimuhusisha Mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Bwana Saidi Mbwana, aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho Mbwana Ally Milandu na Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamili Ally salehe.

Pia mauaji hayo, yameendelea kushamiri na hivi karibuni viongozi wa CCM akiwemo Katibu wa chama hicho, Kata ya Bungu wilaya ya Kibiti bwana Alife Mtulia aliuawa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake, pia Mwenyekiti mstaafu wa CCM wa kijiji cha Muyuni wilaya ya kibiti bwana Idd Kirungi.

Suala la mauaji bado linaendelea kuwaacha watu midomo wazi hususani katika mkoa wa pwani ambapo viongozi na raia wamekuwa wakipoteza uhai wao kwa kupigwa risasi.

IGP Simon Sirro sasa ni wakati wa kutokomeza mauaji mkoani hapo na kuondoa hofu iliyotanda miongoni mwa wananchi wa mkoa huo.

Kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama wa raia visiishie tu kukamata lakini pia, vichungunze kwa makini sababu na kiini cha mtukio ya mauaji hayo.

Halikadhalika serikali inyooshe mkono wake kwa kuvilaani vitendo vya ugaidi na ukatili, ambavyo vinasababisha kupoteza nguvu kazi na viongozi wa taifa letu.




SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa