Tuesday, June 12, 2018

Donald Trump na Kim Jong Un wakutana Uso kwa Uso Singapore

Trump na Kim wameshikana mikono kwa tabasamu

Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore.

Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili hao pekee na wakalimani wao. Kwa sasa, viongozi hao wanakula chakula cha mchana.

Mkutano huu ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.

Trump alisikika akisema kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa haikuwa rahisi kufika hapo.

Mkutano uliokua ukisubiriwa kwa hamu na ghamu ulifanyika katika Hotel ya Capela katika kisiwa cha utalii cha Sentosa.

Viongozi hawa wakiingia katika mkutano walionekana wenye tabasabu, na kusalimiana kwa kushikana mikono, na baadae Kim Jong Un alimshika bega Trumpa kisha wakaanza kuzungumza kwa msaada wa wakalimani wao.

Baadaye washauri na maafisa mbalimbali walitarajiwa kuingia kuendelea na mkutano huku suala la nyuklia likitarijiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana bado makubaliano yatakua yapi.

Akizungumza kabla ta mkutano , katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa umoja wa mataifa utatoa msaada wowote wa kuhamasisha makubaliono katika mkutano huo.

''Viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndio vinabaki kuwa lengo kuu, kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakua na changamoto za hapa na pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote," alisema Guterres.

Mcheza kikapu wa zamani wa NBA, Dennis Rodman amefika Singapore asubuhi ya leo kwa ajili mkutano huo, Rodman ambaye ni rafiki wa kiongozi wa Korea Kaskazini amesema kuwa anafurahia kufika na kushuhudia mkutano huo wa kihistoria.

Source BBC

SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa