Showing posts with label HABARI ZA MITANDAONI. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZA MITANDAONI. Show all posts

Thursday, May 10, 2018

Alichokiandika Haji Manara Baada Ya Simba Kuwa Bingwa wa VPL 2017/ 2018

Alichokiandika Haji Manara Baada Ya Simba Kuwa Bingwa wa VPL 2017/ 2018

Image result for picha za manara

Baada ya mchezo wa leo baina ya Yanga dhidi ya Tanzania Prison, na Prison kuitandika Yanga jumla ya mabao  2- 0, yameitangazia rasmi Simba kuwa mabingwaaa wa  ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara VPL 2017/2018, Haji Manara Afisa habari na mawasiliano klabu ya soka ya Simba  katika ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe ukisema,

" Sifa ziende kwa mwenyezi Mungu mwingi wa rehema muumba mbingu na ardhi niseme nini zaidi ya hapo?
we are......
we are
Haki imecheleweshwa ila Mungu huyu ni wetu sote"


Thursday, May 03, 2018

Alichokisema Haji Manara Baada ya Kupingwa Onyo Kali Na TFF

Alichokisema Haji Manara Baada ya Kupingwa Onyo Kali Na TFF

Related image

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasilianao klabu ya soka ya Simba  Bw. Haji S.Manara Leo amepigwa Onyo  Kali na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi chini ya Mwenyekiti wake Bw. Clement Sanga  kwa kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.

Manara kupitia ukarasa wake wa Instagram ameandika akisema kuwa "Muungwana akivuliwa nguo huchutama, Naomba radhi bodi ya ligi TFF na wadau wote, nilihemewa na furaha ndugu zangu hakuna raha kwangu mimi na kwa mashabiki kama kumgalagaza mtani,, it will never happen again ila sijui itakuwa siku ya kukabidhiwa mwali".


Friday, December 01, 2017

Wema Sepetu Aikimbia Chadema Atangaza Kurudi CCM

Wema Sepetu Aikimbia Chadema Atangaza Kurudi CCM


Muigizaji wa filamu za kibongo na Miss Tanzania 206 Wema Sepetu ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi huku akidai kwamba hawezi kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amesema kwamba anatangaza rasmi kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambacho alitangaza kujiunga nacho Februari mwaka huu.

"Siwezi Kuendelea kuishi kwenye nyumba inayo nikosesha amani... Peace of mind is everything for me. Natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani" . Wema Sepetu.

Thursday, November 16, 2017

Kala Jeremiah Awaomba wanajamii Kumpenda Dr. Luis Shika

Kala Jeremiah Awaomba wanajamii Kumpenda Dr. Luis Shika



Image result for picha za kala jeremiah



Msanii wa muziki wa Hip Hop Kala Jeremiah amefunguka kuwaomba wanajamii kumuonea huruma na kumpenda Dr. luis Shika,

Rapa huyo amefunguka kupitia ukarasa wake wa instagram akisema '' nimesikiliza kwa makini sana maelezo ya mzee wetu sitaki kuongelea utajiri wake wala umasikini wake nataka kuongelea majaribu aliyokutana nayo katika safari ya maisha yake. Ni wazi kuwa mzee huyu yupo Duniani kwa kuwa Mungu kamchagua na mungu humchagua mtu kwa kusudi lake.

nionavyo mimi mzee huyu ni baraka kutoka kwa Mungu haijalishi madhaifu yake ila kwa uhakika ni mpango wa Mungu kuwepo kwake kwetu. Niwaombe wanajamii tumuonee huruma na tumpende hicho ndicho kitu pekee anachohitaji mzee huyu na kwa hakika amekikosa kwa miaka mingi. haitakugharimu chochote kumuhurumia na kumpenda. Nawaomba''


Tuesday, November 14, 2017