Alichokisema Haji Manara Baada ya Kupingwa Onyo Kali Na TFF
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasilianao klabu ya soka ya Simba Bw. Haji S.Manara Leo amepigwa Onyo Kali na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi chini ya Mwenyekiti wake Bw. Clement Sanga kwa kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.
Manara kupitia ukarasa wake wa Instagram ameandika akisema kuwa "Muungwana akivuliwa nguo huchutama, Naomba radhi bodi ya ligi TFF na wadau wote, nilihemewa na furaha ndugu zangu hakuna raha kwangu mimi na kwa mashabiki kama kumgalagaza mtani,, it will never happen again ila sijui itakuwa siku ya kukabidhiwa mwali".
0 comments:
Comment hapa