Pigo Upinzani Baada ya Patrobas Katambi kuhamia CCM, David Kafulila Ajivua Uanachama CHADEMA
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-2015 David Kafulila amejivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Taarifa ya Kafulila kuondoka CHADEMA imetolewa leo kwa vyombo vya habari, na kueleza kwamba hana imani tena na vyama vya upinzani katika kupambana na ufisadi.
David Kafulila anafahamika zaidi kwa kuibua mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa kwa kuibua bungeni suala la Escrow
Kafulila aliwahi kuwa Mbunge kwa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 kupitia chama cha NCCR Mageuzi kabla ya kurudi tena katika chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA hivi karibuni.
0 comments:
Comment hapa