Miili ya wanafunzi,waalimu, na dereva kuagwa leo Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Arusha ambapo leo ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.
Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.
Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hii leo.
Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wamepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa mkoa huo.
0 comments:
Comment hapa