Tuesday, May 23, 2017

Rais Zuma apigwa marufuku na muungano wa wafanyakazi Afrika Kusini

Rais Jacob Zuma apigwa marufuku na COSATU

Baraza la Muungano wa wafanyikazi nchini Afrika Kusini Cosatu ambalo ni mshirika mkuu wa chama tawala cha ANC limempiga marufuku rais Jacob Zuma kuhutubia katika mikutano yake.

Akisoma taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumanne baada ya mkutano mkuu wa baraza hilo, katibu mkuu wa Cosatu Bheki Ntshalintshali alisema: Rafiki Jacob Zuma hataruhusiwa tena kuhutubia katika Cosatu.

Bwana Zuma alizomwa katika mkutano wa wafanyikazi wa mwezi Mei ulioandaliwa na Cosatu mapema mwezi huu.

Chama cha ANC kimegawanyika kabla ya kufanyika kwa mkutano wake wa kila mwaka ambapo rais Zuma anatarajiwa kujiuzulu kama kiongozi wa chama.

Muungano huo ambao ni mkubwa umesisitiza wito wake kwamba haumuungi mkono tena rais Zuma.
Source BBC



SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa