TANZIA: Aliyekuwa mume wa muigizaji Irene Uwoya Afariki Dunia
Aliyekuwa muwe wa zamani wa Irene Uwoya na Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda Bw. Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia usiku wa kuamukia leo.
Kataut beki wa zamani wa Rayon Sports amefariki dunia baada ya kuugua ghafla.
Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza Kataut alikuwa mazoezini jana asubuhi.
Wakati anapoteza maisha, Kataut alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.
Mara ya mwisho, Kataut aliichezea Stand United ya Shinyanga wakati akitokea Cyprus.
Alikuja nchini mara ya mwisho wakati wa Simba Day Agosti 8, akitua nchini Agosti 7 akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kupoteza kwa bao 1-0.
0 comments:
Comment hapa