Tuesday, February 05, 2019

Sunday, February 03, 2019

Simba SC Yaburuzwa Bao 5-0 Dhidi ya  Al Ahly

Simba SC Yaburuzwa Bao 5-0 Dhidi ya Al Ahly



Katika michezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika,  katika kundi D jana ndani mji wa Alexandria Misri kulipigwa mtanange mkali uliozikutanisha timu ya Simba SC ambao walikuwa ugenini kuchuana na Al Ahly.

katika dakika 90 za mchezo huo Simba iliweza kuruhusu alama tatu kwenda kwa timu ya Al Ahly baada ya kukubali kichapo cha bao 5- 0, ambapo magoli yote yalifungwa ndani ya kipindi cha kwanza.

kikosi cha simba kimekuwa na mwendelezo wa kufungwa bao tano kwa sifuru baada ya kupigwa na AS Vita nchini Congo, Simba inaendelea kushika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kundi D ikiwa na jumla ya alama 3 huku Al Ahly ikizidi kujiimarisha kileleni ikiwa na jumla ya alama 7 huku As Vita ikishika nafasi ya pili baada ya jana kutoa sare ya mabao 2- 2 na JS Saoura, na kuifanya JS Saoura iendelea kuburuza mkia katika kundi hilo .

Saturday, February 02, 2019

Friday, February 01, 2019

Mechi Zitakazochenzwa Leo  Ligi Kuu Bara, TPL

Mechi Zitakazochenzwa Leo Ligi Kuu Bara, TPL

Related imageLeo kutalindima michezo minne ya ligi kuu Tanzania bara ambayo itahusisha timu   timu nane zitakazo chuana  kwenye viwanja vinne kutafuta pointi tatu ikiwa ni mzunguko wa pili.

Kagera Sugar watacheza  na kikosi cha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, KMC wapo mkoani Shinyanga watacheza na Stand United uwanja wa Kambarage.


JKT Tanzania wataikaribisha Mwadui uwanja wa Isamuhyo na Ruvu Shooting leo atakuwa kazini kumenyana na Mbeya City uwanja wa Mabatini.