Wednesday, March 22, 2017

Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa

Korea


Maafisa wa ulinzi wa Korea Kusini wamesema Korea Kaskazini ilijaribu kurusha kombora lakini likafeli.

Korea kaskazini ilijaribu kurusha kombora hilo angani kutoka mji wa Wonsan, pwani ya mashariki.
Haijabainika Korea Kaskazini ilijaribu kurusha makombora mangapi au yalikuwa ya aina gani.
Korea Kaskazini imepigwa marufuku kufanya majaribio yoyote ya kurusha makombora au majaribio ya nyuklia na Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, imekuwa ikifanya majaribio mara kwa mara na wataalamu wanasema hilo huenda limeisaidia kupiga hatua pakubwa katika kustawisha teknolojia yake ya makombora.

Mapema mwezi huu, Korea Kaskazini ilirusha makombora manne angani ambayo yalipaa kwa umbali wa kilomita 1,000 na kuanguka maeneo ya bahari yanayomilikiwa na Japan.

Majaribio haya ya karibuni yanaonekana kuwa hatua ya Pyongyang kujibu mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayoendelea kwa sasa kati ya wanajeshi wa Marekani na Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini hutazama mazoezi hayo ya kila mwaka kama maandalizi ya kutekeleza uvamizi dhidi yake.

Jeshi la Marekani pia limethibitisha kwamba liligundua Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kurusha kombora.
Kombora hilo, Marekani imesema, lililipuka sekunde kadha baada ya kurushwa angani.
source BBC

SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa