mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na askari katika jaribio la kupora fedha.
Watu walioshuhudia tukio hilo lililotokea jana Jumapili wamesema mtu huyo akiwa na wenzake walijaribu kupora fedha kwenye gari kabla ya kuwekwa kwenye mashine ya kielektroniki ya kutolea fedha (ATM) ya benki moja iliyopo katika jengo la makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar.
“Aliyekufa aliamriwa asipite barabara hii, alipokataa kusimama polisi walipiga risasi hewani, naye alipotaka kutoa bastola ndipo polisi walipomfyatulia risasi na alikufa papo hapo,” amesema shuhuda wa tukio hilo na kuongeza kuwa
wengine waliokuwa na mtu huyo walikimbia na mmoja amekamatwa.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema atazungumzia tukio hilo leo.
Monday, May 15, 2017
RELATED STORIES
chotamtemi blog inawatakia watanzania wote pasaka njema Chotamtemi.blogspot.com inapenda kuwatakia wata
‘Hedhi si jambo la aibu jamii ishiriki katika kuhakikisha hedhi salama’, wadau wa jinsia. v\:* {behavior:url(#default#VML);} o\:* {behavi
Waziri Mkuu wa Ethiopia kuwasili nchini Leo Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn
LIVE: Kuagwa kwa Miili ya Wanafunzi, Walimu Pamoja na Dereva Katika Ajali Ya Arusha Iliyotokea Tarehe 06/05/2017
Mfanyabiashara Auawa kwa Risasi Singida Mauaji ya kutumia silaha za moto yamee
Rais Magufuli Amtumia salamu za Rambirambi Spika wa Bunge, Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Dr. Elly Marko Macha.
0 comments:
Comment hapa