Friday, August 04, 2017

WAZEE WAZIDI KUPATA SHIDA KWENYE MATIBABU

Katika kuhakikisha wazee wanapata huduma ya afya inayostahili katika hospitali na vituo vya afya wilayani kyela mkurugenzi wa taasisi ya SWOLO Abel Ambakisye amesema kuwa wamefanikiwa kwa kiasi japo kuna changamoto katika baadhi ya vituo.

Akizungumza na kituo hiki ofisini kwake Mzee Abel amesema kuwa wamefikia lengo kwa kiasi kikubwa na wazee wanapata haki ya kutibiwa bila malipo ingawa baadhi ya wahudumu wamekuwa vikwazo kwa wazee pindi wanapohitaji huduma hizo.
 
Hata hivyo, amesema kuwa mfumo wa kutumia vitambulisho vya bima ya afya CHF kama utambulisho kwa wazee bado si rafiki kwao kwani wazee wengi hawana vitambulisho hivyo hali inayopelekea kulipishwa gharama za matibabu

Ameiomba serikali itambue mfumo wa utumiaji vitambulisho vya mpiga kura kwa wazee wakati wakisubiri kujibiwa juu ya ombi la vitambulisho vya utaifa kwa wazee ambavyo havitakuwa na mipaka ya huduma kwa nchi nzima.






SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa