Vigogo watano wa Yanga jijini Mwanza wametangaza kutoa shilingi milioni 30 kwa Toto Africans kama motisha kuhakikisha kuwa wanaifunga klabu ya Simba ili kuipunguza kasi ya ubingwa.
Kwa mujibu wa habari ya gazeti la mwananchi, Msemaji wa Toto Africans, Cuthbert Japhet alithibitisha fedha hizo kutolewa jana kama ahadi kwa wachezaji hao endapo watashinda mchezo dhidi ya Simba.
Matajiri hao ambao pia ni wanachama wa Yanga walisema kuwa timu hizo zikitoka sare, basi watapewa TZS milioni 20. Msemaji huyo alisema kuwa licha ya motisha hiyo lakini wenyewe wanahitaji alama tatu ili kujinusuru kushuka daraja.
Mchezo huo wa leo utakuwa ni wa kuvutia sana sababu Toto watahitaji kushinda kwa namna yoyote ile ili kujinusuru kushuka daraja wakati Simba wao wakihitaji ubingwa kwa nguvu zote ili kufikisha alama 64 na kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.
Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 61 baada ya kucheza michezo 26 wakati Toto wao wapo nafasi ya 15 wakiwa na alama 25 baada ya kucheza michezo 25.
Wakati huo huo, Uwanja wa Mpira wa CCM Kirumba jijini Mwanza umepitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kutumika katika michezo ya kimataifa.
Ratiba ya michezo mingine leo
- Stand United v Mtibwa Sugar
- Ruvu Shooting v MajiMaji FC
- JKT Ruvu v Azam FC Kesho Aprili 16 ;
- Mbao FC v Prisons
- Mwadui FC v Ndanda kimataifa, Kombe la Shirikisho Afrika;
MC Alger v Yanga SC (2:00 usiku)
0 comments:
Comment hapa