Matokeo ya Mechi Zilizochezwa leo na Timu zilizoshuka daraja ligi kuu ya vodacom Bara (VPL)
Leo katika madimba mbalimbali ya Tanzania zimepigigwa mechi tofauti katika ng`we ya kumaliza msimu wa ligi kuu bara (VPL)
ambapo zimepigwa jumla ya mechi nane ambazo ni
1. Prisons vs African Lyon
2. MajiMaji vs Mbeya City
3. Simba vs Mwadui
4. Mbao Fc vs Toto Africa
5. Ndanda Vs JKT Ruvu
6. Stand United vs Ruvu Shooting
7. Azam Vs Kagera Sugar
8. Mtibwa vs Toto African.
katika dimba la taifa ulilindima mchezo kati ya Simba vs Mwadui ambapo Simba walitoka kifua mbele kwa kuicharaza Mwadui FC jumla ya mabao 2- ambapo Simba ndio waliokuwa wa kwanza kutikisa Nyavu za Mwadui katika dakika ya 18 ya kipindiu cha kwanza bao ambalo lilifungwa na shiza kichuya Kwa mkwaju wa penati baada ya kipa shabani wa Mwadui kumgonga Kichuya.
pia kunako dakika ta 25 ya kipindi cha kwanza Ajibu aliiandikia Simba bao la pili baada kugongeana vizuri na Liuzio na kumpa pasi Nzuri Kabisa.
lakini kunako dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza Mwadui walijibu Mashambulizi na kuandika bao Moja, na mpira ulienda mapumziko Simba wakiwa wanaongoza 2-1.
mara baada ya Mapumziko timu zote mbili ziliingia uwanjani kwa nia ya kutafuta goli huku Mwadui wakitafuta kwa udi na uvumba Bao la pili la kusawazisha lakini jitihada zao hazikuweza kuzaa matunda na mpira uliisha Simba wakitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-1.
Lakini Pia katika Dimba la CCM Kirumba ulilindima mchezo baina ya Yanga FC na wakata mbao Mbao FC ambapo kwa mara ya pili mfululizo Yanga inabebeshwa Mzigo wa Mbao dhidi ya wakata mbao. Ambao Mbao wametoka kifua mbele kwa kucharaza Yanga FC bao 1-0 bao ambalo lilifungwa kipindi cha kwanza.
Matokeo kwa ujumla ya mechi zilizochezwa ni
Mbao 1 - 0 Yanga
Simba 2 - 1 Mwadui
Azam 0 - 1 Kagera Sugar
Mtibwa 3 - 1 Toto
Maji Maji 1 -1 Mbeya City
Stand United 1 - 0 Ruvu Shooting
Prisons 0 - 0 Lyon
Ndanda 2 - 0 Jkt
Mara baada ya michezo ya Leo Timu za African Lyon ya Dar Es Salaam , Toto African ya Mwanza na JKT Ruvu ya mkoani Pwani ndizo zimeshuka Daraja.
0 comments:
Comment hapa