Wednesday, May 17, 2017

Serengeti Boys Uso kwa Uso na Angola


kesho timu ya Taifa ya vijana  chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys wanakitupa uwanjani kwa mechi yao ya pili dhidi ya Angola  wamesema wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo ya michuano ya Afcon dhidi ya Angola..

Ambao awali  katika mechi ya kwanza walianza kwa sare ya bila mabao dhidi ya Mali.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema wana majeruhi mmoja na wachezaji waliobaki wamejiandaa vya kutosha.

“Kwa kweli tumejiandaa vizuri na tunataka kupata ushindi wetu wa kwanza. Kila mmoja anajua haitakuwa kazi rahisi lakini tutapambana vilivyo,” alisema.

Boys wako katika Kundi B na timu za Mali, Angola na Niger.

SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa