Sunday, June 25, 2017

Taifa Stars Kumenyana na Malawi Leo, COSAFA Afrika Kusini


Timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars leo inashuka dimbani Afrika kusini katika mchezo wao wa kwanza wa kundi A kumenyana na timu ya taifa ya Malawi katika mashindano ya COSAFA.

Mchezo kati ya Taifa Stars na Malawi unachezwa kwenye Uwanja wa Moruleng mishale ya saa 9:00 za mchana za Afrika Kusini lakini kwa saa za East Africa itakuwa ni saa 10:00 jion na kufuatiwa na mchezo wa pili kati ya Ushelisheli na Angola utakaochezwa mishale ya saa 11:30 za jioni kwenye Uwanja huohuo.


Tanzania imepangwa kundi A pamoja na timu za taifa za Malawi,Ushelisheli pamoja na Angola.Mshindi wa kwanza wa kundi A atafuzu robo fainali na kucheza na wenyeji Afrika Kusini ambao pia ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Tanzania imealikwa kushiriki michuano ya COSAFA ya mwaka huu kuchukua nafasi ya Comoro iliyojitoa katika dakika za mwisho kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

Michuano ya kombe la COSAFA CASTLE imepangwa kuanza kutimua vumbi lake Juni 25 na kuishia Julai 9 ambapo jumla ya timu 14 zitachuana kumsaka mshindi mmoja.

Michuano ya COSAFA huandaliwa kila mwaka na baraza la mpira wa miguu la nchi za kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa kushirikiana na kampuni ya kutengeneza vinyaji vikali ya Afrika Kusini ya Castle Lager.

Kikosi cha Taifa Stars ambacho kitashiriki michuano ya COSAFA CASTLE ni makipa Aishi Salum Manula (Azam FC),Benno David Kakolanya (Young Africans SC) na Said Mohammed Said
(Mtibwa Sugar FC).

Mabeki ni Shomari Salum Kapombe (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan
‘Kessy’ (Young Africans ) Gadiel Michael (Azam FC),Hamim Abdulkarim (Toto
Africans FC).

Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Hassan Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons).

Viungo ni Himid Mao Mkami (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC,Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).

Washambuliaji ni Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna-Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar),
Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC

SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa