Thursday, November 16, 2017

TFF Yakanusha Tuhuma za viongozi wake kujilipa Posho Za Mamilioni




 Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umekanusha juu ya taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa mitandaoni zikiwahusu viongozi wa shirikisho hilo wakiongozwa na rais wao, Wallace Karia kujilipa posho ya kiwango cha juu.

 viongozi wa kuchaguliwa TFF hawapati mishahara, badala yake wanalipwa posho, sasa ilielezwa kwamba Karia analipwa Sh milioni sita, makamu wake Sh milioni tano huku wajumbe wa Kamati ya Utendaji wakilipwa milioni moja kwa kila mwezi.

Hayo yameelezwa leo wakati Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao akizungumza na waandishi wa habari na  kukanusha taarifa hizo na kusema kuwa ,  suala hilo halina ukweli na kudai kuwa Karia alikataa kulipwa na kusisitiza posho yake ipelekwe katika masuala mingine ya kimpira kwa kuwa yeye ni muajiriwa wa serikalini na analipwa mshahara huko.

“Hizo taarifa hazina ukweli wowote kwa sababu viongozi wa hapa hakuna ambaye anachukua kiasi hicho cha fedha.


“Hata kwenye suala la wajumbe, nao hakuna ambaye anapokea shilingi milioni moja kwa mwezi kama inavyosemekana badala yake tunatoa shilingi milioni moja na nusu kwa miezi mitatu tena kwa yule ambaye anachakarika na tunaona juhudi zake kwa kupitia ripoti ambazo anawasilisha kwenye vikao.


“Lakini kwa sababu jambo hilo limechafua sura ya taasisi yetu tuna mpango wa kuwafungulia kesi ya makosa ya kimtandao wale wote ambao wamehusika kwenye suala hilo na tayari tuna majina 10 ya watu ambao tutaanza nao,” alisema Kidao.



SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa