Leo katika mzunguko wa 10 ligi kuu Tanzania bara VPL kumerindima mchezo katika dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam, ni mchezo ambao uliwakutanisha wagonganyundo wa Mbeya, Mbeya City ambao walichuana vikali na wana jangwani Dar young Africans, Yanga.
katika mchezo huu Yanga imewagonga nyundo wagonga nyundo hao kwa mikwaju ya mgoli matano (5) huku Mbeya city hawakuambulia kutikisa nyavu za lango la yanga.
katika kipindi cha kwanza Yanga ilitoka mapumziko ikiwa inaongoza mbele kwa mabao mawili kwa 0 ni mabao bao la kwanza lilifungwa na Chirwa kunako dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza kutokana na uzembe wa walinzi.
lakini pia kunako dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza yanga waliongeza kukonga nyundo kupiti mchezaj wao Emmanuel Martine ambaye aliwatoka walinzi wa Mbeya City na kufunga.
baada ya mapumziko Mbeya city walionekana kulemewa sana kitika mchezon na kunako dakika ya 50 ya kipindi cha pili Chirwa alipiga penalti nzuri, ilijaa wavuni, penati iliyopatikana baada ya mchezaji Raphael Daudi kufanyiwa madhambi kwenye penalt box.
Lakini pia kunako dakika ya 59 Chirwa aliipatia Yanga bao la nne akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu, dakika ya 80: Yanga walipata bao la tano, kazi nzuri ya Gadiel Michael alimpa pasi Martine ambaye alifunga bao kwa shuti kali.
Mashabiki wa mbeya city walitoka uwanja wakiwa modomo wazi hakuamini kilichotokea pale katika dimba la Uhuru.
Hat-trick ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa ni ya pili kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya Emanuel Okwi kufanya hivyo (Okwi alifunga goli 4) kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi August 26, 2017 Simba ilipocheza dhidi ya Ruvu Shooting.
matokeo mengine ya michezo iliyochezwa leo
Azam 1- Njombe Mji 0
Kagera 1- Mtibwa 0
0 comments:
Comment hapa