Maneno ya Haji Manara Kwa Waamuzi Watakaochezesha Mchezo Wa Simba Vs Yanga 29, April, 2018
Kufuatia mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara VPL, utakao wakutanisha watani wa jadi Simba Vs Yanga katika dimba la taifa tarehe 29, April, 2018, uongozi wa klabu ya soka ya Simba umesema kuwa unaamini waamuzi waliopangwa kuchezesha mchezo huo watafata sheria zote 17 za soka na kufanya haki itendeke.
Hayo yamebainishwa wakati Afisa habari wa klabu hiyo Bw. Haji Manara alipozungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi kariako, ambapo alisema kuwa “Waamuzi watakaocheza tunaamini watafuata sheria 17 za soka kwa ajili ya kufanya haki itendeke,”
Mbali na hapo Bw. Manara aliongeza kwa kusema kuwa Simba na Yanga si Mahasimu wa jadi bali ni Watani wa Jadi na kusema kuwa neno hilo halipaswi kutumika katika vyombo vya habari.
0 comments:
Comment hapa