Monday, April 23, 2018

Mohamed Salah Ajinyakulia Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa England 2017/ 2018



Mchezaji nyota wa klabu ya soka ya Liverpool Mohamed Salah ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka England kwa musimu 2017/ 2018 tuzo hiyo maarufu kama PFA player of the year jana ilimtangaza Mchezaji huyo kuwa mshindi wa tuzo hiyo.

Mchezaji huyo ameishinda tuzo hiyo kutokana na kiwango cha soka alichokionesha kwa musimu huu, Salah anashinda tuzo hiyo akiwa kaichezea timu yake jumla ya michezo 46 na kuwa na jumla ya magoli 41 na assist 13 kwa musimu huu,

Pia alipohojiwa na vyombo vya habari nchini humo Salah alisema kuwa anafurahi sana juu ya ushindi wa tuzo hiyo na kusema  siku zote anaiwazia klabu yake ushindi pia anawaza kushinda kwa ajili ya klabu yake.

Endelea kufatilia chotamtemi blog kwa habari za kimichezo, siasa, burudani, ndan na nje ya nchi.

SHARE THIS

0 comments:

Comment hapa